Nay wa Mitego hajafungiwa kufanya show

Nay wa Mitego hajafungiwa kufanya show

Baada kuzuka sintofahamu kupitia mitandao ya kijamii kuhusiana na suala la msanii wa hip-hop nchini Nay Wa Mitego kufungiwa kufanya show.

Kupitia mahojiano ya na moja ya chombo cha habari Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana ameeleza kuwa hawakumfungia Nay kupiga show bali walimuita ili kuzungumza naye.

Katika ukurasa wa Instagram wa mwanamuziki huyo ameshare video ikimuonyesha katibu mtendaji huyo akizungumza kuhusiana na yeye kutokufungiwa ikiambatana na ujumbe usemao,

“Changamoto zipo kwa ajili ya kutuimalisha zaidi. sasa wana nchi wangu wa njombe na makambako jiandaeni rais wenu nakuja kuonana nanyi tarehe 30 mwezi huu njombe na tarehe 1 ni makambako.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags