Nandy: Nianze na sura au jina la mtoto

Nandy: Nianze na sura au jina la mtoto

Ahoooohweeeeh! Haya haya mji ushaanza kuchangamka uko, mambo yameshakuwa mengi muda mchache, basi bwana baada ya kusubiriwa kwa kipindi kirefu na watu kuwa na shauku ya kumuona mtoto wa The African Princess Nandy sasa  yupo tayari kuwaonesha binti yake.

Kufuatia ukurasa wake wa Instagram Nandy ameacha swali kwa mashabiki zake na kuwauliza mwezi huu aanze na kuiweka wazi sura ya mwanae au aanze na jina, ambapo ujumbe huo ulikuwa umeandikwa kama ifuatavyo…

“Mwezi huu ni mwezi wangu jamaani, mwezi wa shughuli!!! sijui tuanze na jina la mtoto au sura, hii April ya Nandy nauanza mwezi wanne kwa kasi ya ajabu” ameandika Nandy

Haya haya wanangu sana vipi kwa upande wenu mnataka lianze jina au sura dondosha komenti yako hapo chini, bila kusahau kufuatilia mitandao yetu ya kijamii @Mwananchscoop  kwa updates Zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags