NANDY NA BILLNASS: Kutoka kudate, kuwa ma-EX, kupigwa block, video kuvuja, mimba, mpaka ndoa

NANDY NA BILLNASS: Kutoka Kudate, Kuwa Ma-EX, Kupigwa Block, Video Kuvuja, Mimba, Mpaka Ndoa

Hayawi hayawi na sasa yamekuwa... wasanii maarufu nchini Tanzania, Faustina Mfinanga 'Nandy' na William Lyimo 'BillNass' wamefunga pingu za maisha, Jumamosi hii ya tarehe 16/03/2022. Wawili hao wamekuwa kwenye mahusiano kwa miaka 6, na hatimae safari yao imezaa matunda, ila unaijua vizuri historia yao? Toka kujuana 2015, kuanza mahusiano 2016, kuachana na Nandy kuchumbiwa na Marehemu Ruge, video yao kuvuja, kurudiana, kupeana mimba na hatimae kufunga ndoa, historia ya hawa wawili ni ya aina yake, kwani inasisimua kwa mabonde na milima waliyopitia.Nandy na Billnass wamedumu kwenye uhusiano kwa muda mrefu lakini ukiwa ni uhusiano uliotafsiriwa kuwa wa ‘in and out.’ Wawili hao walisoma chuo kimoja cha CBE, ingawa maongezi yao yalianza katika mashindano ya muziki ya TECNO. Billnass akaslide DM ili kumpongeza Nandy kwa uimbaji mzuri, ingawa Nandy hakujibu mpaka siku anayorudi Tanzania, ambapo Billnass alimpongeza tena kwa kuwa mshindi wa pili.Ilikuwa ni mwaka 2015, ambapo Billnas akatusua kupata namba ya Nandy. Baada ya kufanikiwa kupata namba yake, ndipo mawasiliano yalipoanza, ila haikuwa hadi mwaka 2016 ambapo wawili hao walianza kudate kwani mwaka 2015, kila mtu alikuwa na mtu wake.

WALIKOTOKA

Wawili hao ambao waliwahi kufunguka kuwa kwa mara ya kwanza waliandika ukurasa wa kimapenzi katika tour ya tamasha maarufu la Fiesta lililofanyika mkoani Mbeya mwaka 2016, wamepitia milima na mabonde mengi.

Nandy ana describiwa kama mtu mfuatiliaji na mwenye wivu, kama ambavyo BillNass alisema kupitia interview yao moja na mtangazaji Millard Ayo. Mwaka wao wa kwanza kudate haukuwa na furaha sana kama ambavyo wengi wangetarajia na hiyo iliwafanya wawili hao kuvunja uhusiano wao. Bill Nass aliconfess kuwa huwa alikuwa anampiga block sana Nandy, hadi kufikia hatua ya kumpiga block yeye na familia yake nzima pamoja na page zozote zile zilizokuwa zinampost Nandy.


MISUKOSUKO KATIKA MAHUSIANO
Kila mahusiano hayakosi misukosuko na uhusiano huu sio tofauti.

  • KUKATALIWA UKWENI

Kulikuwa na tetesi ya suala la kukataliwa ukweni, ingawa Billnass aliwahi kukanusha na kudai kuwa ni maneno ya mtandaoni. “Kuhusu kukataliwa ukweni, sidhani kama ni kweli, lakini pia wakwe zangu mimi ni watu wa dini sana, hivyo nisingependa kuwaongelea sana kwenye media yoyote ile kwa sababu ninachokijua mimi ni kwamba, wananipenda kama mtoto wao na wamenikubali,” alisema Billnass alipozungumza na gazeti hili mwaka jana.

Julai 25 mwaka 2020, Dada Nandy aliweka wazi kuwa bado ni mapema sana kwa mdogo wake kuolewa.

“Bado kwa mimi na familia yetu, tunaona kuwa Nandy muda wa kuolewa bado, hata mimi nilikaa uchumba miaka mingi, mpaka ninakuja kuolewa… kwa sababu ndoa ya kikristo hamuachani labda mkimbilie mahakamani. Kwa hiyo mtu anatakiwa kukaa na kufkiria ili msikurupuke,” alisema.

Kauli hiyo ya Dada yake Nandy ilikuja miezi michache baada ya Billnass kumvisha pete Nandy. Billnass alimvisha pete Nandy Aprili 10 mwaka jana katika hafla ambayo ilihudhuriwa na ndugu wachache.

 

  • KUPAMBANA NA UMAARUFU

Wachambuzi wa masuala ya kisaikolojia na kimahusiano, walidai umaarufu wa Nandy ambao ni dhahiri amemzidi Billnass vilevile unaweza kuwa chanzo cha wawili hao kuachana.

Mmoja wa watalaam hao, Mr. Kidee alisema dalili za kuyumba kwa mahusiano ya ambayo mwanamke anaonekana kuwa nguvu aidha ya kiuchumi, au umaarufu kuliko mwenzie huonekana dhahiri. Alisema hali hiyo inaweza kujitokeza iwapo wawili hao hawatokuwa wamejenga mahusiano yao katika misingi imara.

Alitolea mfano uchumba wa Nandy na Billnass ambao ulionekana kulegalega tangu awali na kuongeza kuwa ni jambo ambalo halikuwashtua wengi ingawa mashabiki walitamani wawili hao wadumu pamoja.

Hata hivyo, baada ya kuachana, Nandy alitangaza baada ya kifo cha aliyekuwa mmoja wa wamiliki wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, kuwa alitakiwa kutolewa posa miezi michache hapo mbeleni. Ambapo katika interview moja wapo wakiwa wanapromote nyimbo ya "BUGANA," BillNass alimwambia Nandy kuwa kama watarudiana basi atamuoa.KUVUJA KWA VIDEO MBAYAKatika mahusiano ya hawa wawili, kwenye kipindi ambacho walikuwa wamebreak up,  video ya wawili hao wakiwa faragha ilivuja, kitendo kilichowachanganya wote wawili. "Nililia," BillNass alisema. Hata hivyo, baada ya kuingia kwenye mikono ya sheria, uchunguzi ulifanyika na hatimae waliweza kuwapata watu waliohusika katika usambazaji wa video ile, ila Marehemu Ruge aliwaomba wasamehe na walifanya hivyo.Baada ya kifo ya Ruge, wawili hao walirudisha ukaribu wao hadi walioamua kurudisha tena majeshi, na BillNass alimvalisha pete ya uchumba Nandy katika tamasha moja.


ENGAGEMENTMungu si Athuman wala Rama, BillNass akafanya yake na kuja kutoa mahari kwa wapare. Sherehe ilifanyika ya kufana sana na wawili hao wakawa wameanza safari mpya ya maisha.

UJAUZITO


Mnamo mwaka huu, kulitokea tetesi nyingi juu ya Nandy kuwa mjamzito, tetesi hizo zilikuja kuthibithishwa baadae sana kupitia page zao za Instagram ambapo walipost picha zao za maternity photoshoot.

NDOABillNass pamoja na Nandy walifunga ndoa, Jumamosi, 16/07/2022 katika kanisa la kiLutheri, Mbezi na sherehe kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City. Ndoa yao ilihudhuriwa na mastaa kibao. Maharusi hao walipatiwa zawadi ya zaidi ya milioni 200 na gari juu. Huu ni mfano hai wa alipangalo Mungu, mwanadamu hawezi kulitenganisha.

All the best katika maisha haya mapya ya ndoa na kuwa wazazi.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post