Namna ya kutupia na vazi la blazer

Namna ya kutupia na vazi la blazer

Wanangu niaje? It’s another Friday katika fashion ndani ya Mwananchi Scoop. This Friday tutaangazia katika vazi la Blazer na mitindo yake tofauti tofauti katika mitupio yako ya weekend au ofisini na kuonekana nadhifu.

Blazer ni aina ya jacket au koti ambalo kwa kawaida siyo lazima kuvaliwa kwa mtindo wa suti lakini humfanya mvaaji kuonekana nadhifu.

Licha ya kuwa siyo vazi rasmi, blazer ikipangiliwa kwa ustadi inaweza kuvaliwa mahali popote panapofanyika shughuli rasmi kama mikutano au semina, ofisini na mitoko mingine.

Katika kipindi cha majira ya mvua mtindo huo ndiyo wakati wake, hasa kwa wanawake kutokana na aina nyingi ya nguo walizonazo kuacha wazi sehemu kubwa ya miili yao hivyo hutumia kwa ajili ya kujikinga na baridi na kumfanya mvaaji kuonekana nadhifu na kujiamini.

Wabunifu wa mavazi wanasema kwamba kulingana na hali ya hewa ya sasa, maeneo mbaliimbali nchini blazer inaweza kuwa mkombozi na kumfanya mwanamke kuonekana wa kisasa.

NAMNA BLAZER INAVYOWEZA KUVALIWA

Gharama za makoti ya mtindo huu zinatofautiana kulingana na eneo husika na uhitaji wake au mvaaji kwa kuzingatia malighafi iliyotumika katika kutengeneza. Nguo ya blazer inaweza kuwa katika mtindo wa namna mbili inaweza kuwa blazer ndefu ambayo inafanana na vazi au inaweza kuwa blazer fupi. 

  • Blazer inaweza kuvaliwa na sketi fupi
  • Suruali ya jeans au ya kitambaa
  • Gauni

Blazer inatakiwa kupangilia rangi lakini koti la mtindo huu linaweza kwenda vizuri na kupendeza na nguo yoyote kwa kiatu kirefu au raba.

MITINDO YA MAVAZI YA BLAZER 

Linapokuja suala la mitindo ya nguo za blazer, kuna aina mbalimbali za kuchagua namna ya kutupia kama;

  • Sleeveless

Nguo nyingi za blazer zina mikono mirefu ambazo huvaliwa na vest ndani na blazer zisizo na mikono huvaliwa na t-shirt au shati ya mikono mirefu.

Hupendeza zaidi katika majira ya joto.

Vilevile blazer inaweza kuwa na vishikizo ambavyo mvaaji anaweza kuvifunga au kuviachia, vishikizo hivyo hufanya kazi kutenganisha sehemu ya juu na ya chini huku ikidumisha urembo.

  • Mkanda

Nguo za blazer pia zinaweza kufungwa mikanda kulingana na nguo uliyovaliwa katika kuongeza urembo au umaridadi katika vazi husika, mara nyingi mtindo huu hutumika zaidi katika vazi la gauni au sketi fupi.

  • Mipasuko

Blazer ndefu mara nyingi huwa na mpasuo unaomfanya mvaaji kuwa na muonekano wa kuvutia katika vazi lake.

Pia zina uwezekano mkubwa wa kupatikana kwenye mitindo ya aina ya mavazi tofauti tofauti hupendelewa kuvaliwa zaidi na suruali za vitambaa au jeans.

Hilo ndo vazi la blazer bhana. Je utaongeza moja kwenye kabati

lako ili kwenda na wakati katika mitoko yako?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post

Latest Tags