Namna ya kukabiliana na migogoro isio ya lazima katika ndoa na mahusiano

Namna ya kukabiliana na migogoro isio ya lazima katika ndoa na mahusiano

Haya haya kumekucha kama kawaida yetu kila siku lazima kushauriana na kuambiana mawili matatu kuhusiana na mahusiano, sasa leo nimekuja na jambo konki ambali hili ndo chanzo haswa cha mahusiano mengi kuvunjika, hii ni kwasababu ya maugomvi na migogoro isio ya lazima.

Mawasiliano mabovu au kutokuelewana hii ndio changamoto kubwa sana katika ndoa na mahusiano ndio chanzo cha taraka nyingi kwa mujibu takwimu za hivi karibuni zinasema kuwa ndoa nyingi zinavunjika kutokana na migogoro isio ya lazima.

Kimsingi ni kwamba migogoro inayosababishwa na kutoelewana chanzo chake kinaweza kuwa ni mmoja au wote wawili. Migogoro kikawaida ipo kwenye ndoa zote ila hutofautiana kwa kiwango.

Ipo kwenye kila ndoa kutokana na sababu za malezi na tabia za asili za wanandoa. Na kawaida migogoro ukua kutokana na kukosa utayari wa kuitatua kwa wanandoa wenyewe ama kwa wote wawili au mmoja wao.

Migogoro ya kutoelewana ipo inayotokana na mahitaji ya kawaida na ya kimwili, Leo tutaongelea migogoro inayotokana na mahitaji ya kawaida  nina maana mahitaji ya msingi ya binadamu kama vile chakula, mavazi , kumpendezesha na kumthamini.

  • Kuwa mkweli kuhusu hali ya kipato chake.

Kuwa mkweli wa hali yako kiuchumi yaani kuwa mkweli kwa mwenza wako kuhusu hali ya kipato chako na ukweli huu ni vizuri ufanyike kabla ya kufunga ndoa, Ni vizuri sana kama utauvaa uhalisia wako kipato kipindi chote cha uchumba. Hili, ni muhimu sana kwa sababu itakusaidia kujua kama mchumba wako ni wa kiwango chako au laa,  Ukidanganya katika suala hili unakuwa umepande mgogoro ambayo itakuwa vigumu kuusuluhisha na unakuwa umejenga hali ya kutoaminika. 

  • Onyesha kujali hitaji la mwenza wako.

Jitahidi kujali mahitaji ya mwenza wako kwa kumtimizia hitaji lake kama uwezo unaruhusu na kama unaona sihitaji la msingi, tafuta lugha nzuri ya kumweleza ni kwa nini unaona hitaji lisitimizwe na bila kuonyesha dalili za kupuuza au kuonyesha sihitaji la msingi. Kingine kama hitaji ni lamuhimu haswa na pesa huna kwa muda huo inabidi utafute namna nzuri ya kumueleza kuwa kwa wakati huo huna pesa ila ukipata tu utamtimizia

  • Epuka ahadi za uongo

Jitahidi sana kuepuka ahadi za uongo hii huleta migogoro isiyo ya lazima kwasababu watu wengi huweka ahadi walizo pewa kichwani mwao kuliko jambo lolote, so inabidi pale tu unapo ahidi kumtendea jambo basi hakikisha umelitimiza kwa namna yoyote.

  • Epuka kuonyesha upendeleo kwa wageni wanao watembelea nyumbani.

Ni jambo la kawaida sana ndugu wa pande zote kutamani kuwatembelea wanandoa katika hali ya amani au matatizo. Ni vizuri kujitahidi kutoonyesha unyanyapaa kwa wanandugu wa upande mmoja hali hii inaweza kuleta mgogoro mkuu.

  • Epuka kuonyesha dharau dhidi ya mila na desturi za mwenza wako.

Inapotokea wanandoa ni makabila tofauti ina maana watakuwa wamekulia kataika mila na desturi tofauti. Mila na desturi uhusisha namna ya kuongea, mapishi, tofauti za kimaendeleo baina ya kabila moja na nyingine. Si vizuri kuonyesha dharau hata kama ni katika hali ya utani kwa sababu hiyo huonyesha hisia zako dhidi ya mwenzako hata kama utasema unamtania.

  • Epuka utani wa kimaumbile.

Jitahidi kuepuka utani unaohusiana na maumbile kama vile watu wafupi au wanene wana kasoro 1,2,3 n.k. wakati ukijua kwamba mwenza wako nao ana maumbile kama hayo. Utani kama huo hufanya mtaniwa kujisikia vibaya na kuleta migogoro katika ndoa.

  • Epuka kuonyesha upendeleo katika kusaidia ndugu. 

Katika familia zetu za kiafrika kuna matatizo ya kila namna kwenye familia zetu yaani; kwa upande wa mke na mwanaume. Inapotokea kuna mahitaji upande wa familia za upande mmojawapo ni muhimu sana kuweka uwiano wa misaada inayotolea, ili kuepuka kuonyesha upendeleo.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post