N’golo Kante aungana na Benzema, Al Ittihad

N’golo Kante aungana na Benzema, Al Ittihad

Klabu ya Al Ittihad ya Saudi Arabia bado inaendelea kushusha vyuma na sasa imetangaza kumsajili kiungo N’Golo Kanté ambae ni raia wa Ufaransa kwa uhamisho huru kutoka Chelsea.

Kupitia taarifa yake kwa umma Al Ittihad FC imefichua kuwa Kante amesaini mkataba wa miaka mitatu, huku mwamba huyo atatia kibindoni mshahara wa Euro milioni 25 ni sawa na Zaidi ya billion 60 za kitanzania kwa mwaka sambamba na atavaa jezi namba 7.

Ujio Kante klabuni unakuja wiki chache baada ya nyota wa zamani wa Real Madrid, Karim Benzema kujiunga na miamba hiyo yenye maskani yake Jeddah mapema mwezi huu.

Katika video iliyosambazwa mtandaoni na klabu hiyo, Benzema alimpongeza Mfaransa mwenzake, akisema, “Kuna wakati niliwahi kukuambia, wewe ni mchezaji “box to box” bora zaidi duniani. Sasa nina furaha kucheza na wewe tena, na bila shaka katika timu bora nchini Saudi.” Alisema Benzema






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags