Mwili wa mwanamitindo maarufu Chiloba kuzikwa leo

Mwili wa mwanamitindo maarufu Chiloba kuzikwa leo

Mbunifu wa mitindo na mwanaharakati wa LGBTQ, Edwin Chiloba atazikwa leo katika Kijiji cha Sergoit.

Marafiki na familia ndio wamechukua mwili kutoka katika chumba cha kuhifadhia maiti cha MTRH. Msemaji wa familia amesema kila mtu anakaribishwa nyumbani kutoa heshima zake za mwisho.

Gaudencia Tanui ambaye ni msemaji wa familia amesema ana matumaini kwamba wauaji wa Chiloba watafikishwa mahakamani na kupata stahiki yao.

Washukiwa 5, akiwemo rafiki wa muda mrefu wa Chiloba, wako rumande huku polisi wakikamilisha uchunguzi kabla ya kufunguliwa mashtaka rasmi.

Tanui pia amewaeleza waandishi wa habari kwamba familia hiyo imeshtushwa na habari za mitandao ya kijamii zinazoelekezwa kwa familia yake, ambazo alisema ziliwaacha wakiwa na huzuni sana.

Aidha anatumai chuki yote haiondoi ukweli kwamba uhalifu umetendwa na haki lazima ipatikane.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post