Mwijaku, Nandy Alitaka kunilipa Million 1.8 nimchafue Zuchu

Mwijaku, Nandy Alitaka kunilipa Million 1.8 nimchafue Zuchu

Aloooooooh! Huku mjini Instagram bwana kuna sakata ambalo linaendelea linalo muhusisha bibi harusi wetu wa juzi kati Nandy na yule Dc wa Instagram Mwijaku baada ya kuvuja kwa sauti ya Mrs Nenga kumpa maelekezo Dc huyo kumchafua Zuchu.

Basi bwana Mwijaku baada ya kusikia sauti zinazo samba aliamua kuuvunja ukimya na kueleza kuwa “ Nandy alitaka kunilipa million 1.8 ili niweze kuposti kupitia ukurasa wangu kwa ajili ya kumchafua Zuchu, mimi nikamwambia hapana siwezi nikapokea pesa ili nimchafue mtu” aliendelea kwa kusema

Zuchu ni kijana mdogo anapambana kwenye kuimba na anaimba vizuri kwahiyo kwenye dili zenu ndogo mimi mkiniingiza mtakuwa mnanikosea na hiyo sauti inayosambaa mtandaoni ni kweli ya Nandy ni  ya mwaka 2021 akinitaka nichafue Zuchu” amesema Mwijaku

Mambo si mambo kwakweli haya wadau wa Mwananchi Scoop mnalizungumziaje hili swala je ni sawa kumlipa mtu ili kumchafua mtu? Dondosha komenti yako hapo chini.






Comments 1


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags