Mwigizaji Donald Sutherland, kutoka nchini Canada aliyejulikana kupitia filamu zake kama ‘The Hunger Games’ na ‘MASH’, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Taarifa ya kifo chake imetolewa na mtoto wake aitwaye Keifer huku akimuenzi baba yake kwa kumsifu kuwa ni mwigizaji muhimu katika historia ya Marekani.
“Kwa moyo mzito, ninakuambia kwamba baba yangu, Donald Sutherland, ameaga dunia. Binafsi nadhani mmoja wa waigizaji muhimu katika historia ya filamu, lipenda alichofanya na kufanya kile alichopenda” alisema mtoto wa marehemu mwigizaji Sutherland
Donald Sutherland alizaliwa Julai 17, 1935 na kufariki siku ya jana Juni 20, 2024 nyumbani kwake jijini Miami, Florida, nchini Marekani alipokuwa akiishi na familia yake.
Mwigizaji huyo aliwavutia mashabiki wengi katika filamu za kivita zikiwemo ‘Kelly's Heroes’, ‘Forsaken’ ‘The Eagle Has Landed’ huku akikabidhiwa nyota ya heshima ya ‘The Hollywood Walk Of Fame’ mwaka 2011 kufuatia na mchango wake wa kukuza tasnia ya uigizaji.
Leave a Reply