Mwanasiasa Peter Obi atajwa kuingilia kati ugomvi wa P-square

Mwanasiasa Peter Obi atajwa kuingilia kati ugomvi wa P-square

Mwanasiasa kutoka nchini Nigeria, Peter Obi ameripotiwa kuingilia kati ugomvi wa wanamuziki Paul na pacha wake Peter Okoye, hii ni baada ya kuonekana nyumbani kwa RudeBoy siku ya jana Agosti 13, 2024.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa RudeBoy ameshare video ikimuonesha mwanasiasa Peter Obi na kaka mkubwa wa mapacha hao Jude Okoye huku akiambatanisha na ujumbe wa shukurani kutoka kwa mwanasiasa huyo licha ya kutokuwekwa wazi sababu ya Obi kufika nyumbani kwa RudeBoy.

Aidha kufuatia na video hiyo wadau na mashabiki mbalimbali walifurahishwa na ziara hiyo ya Obi kwani huenda ilikuwa ni kwa ajili ya kulirudisha tena kundi la P-Square lililowahi kutamba na ngoma kama ‘Taste The Money (Testimony)’, ‘Personally’, ‘Forever’ na nyinginezo.

Ikumbukwe kuwa Agosti 2, 2024 Paul Nonso Okoye ‘Rudeboy’ alithibitisha kuwa kundi la #PSquare limegawanyika kwa mara nyingine kwa kudai kuwa toka walivyoungana hakuna cha maana kilichowahi kufanyika.

Aidha kwa upande wa kaka yake Peter Okoye ‘Mr P’ alituma barua ya wazi kwa ndugu yake huyo kwa kumtaka aachea kupotosha umma kwa kudanganya kuwa yeye ndio aliyekuwa akihusika kwenye kila kitu katika kundi hilo.

Hata hivyo mpaka kufikia sasa ugomvi wa wawili hao bado haujafikiwa muafa huku baadhi ya wanasiasa na watu mashughuli wakitolea maoni suala hilo na kuitaka familia ya Okoye kuwasuluhisha wawili hao mapema kabla hawajachelewa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags