Mwanasheria wa Diddy afunguka sakata la kuwekwa chini ya uangalizi

Mwanasheria wa Diddy afunguka sakata la kuwekwa chini ya uangalizi


Baada ya kuzuka kwa taarifa siku ya jana kuwa mwanamuziki Diddy yupo chini ya uangalizi wa kuzuia kujiua, Mwanasheria wa rapa huyo Marc Agnifilo afunguka kuhusu sakata hilo huku akidai kuwa mteja wake hafikirii kujiua hata kidogo.

Akizungumza na Tmz, Marc ameweka wazi kuwa kwa sasa Diddy yupo imara na mwenye afya, kwani amewekeza akili yake kwenye kulisafisha jina lake Mahakamani.

“Nimetumia masaa kadhaa na mwanzilishi wa ‘Bad Boy Entertainment’ akiwa chini ya ulinzi wa serikali nimeona kuwa hana mawazo ya kujiua hata kidogo, yupo imara, mweye afya na nina uhakika ameweka akili yake kwenye kujitetea na kusafisha jila lake mahakamani.” Amesema Marc

Mbali na hilo baadhi ya vituo vya redio na Tv vimeamua kusimamisha kupiga muziki wa Sean 'Diddy' Combs baada ya kukamatwa kwake na kukabiliwa na Mashitaka mbalimbali.

Kwa mujibu wa TMZ imesema mashirika mengi ya redio na stesheni nyingi huko Marekani na maeneo mengine yamepiga marufuku kuchezwa kwa muziki wa msani huyo, huku baadhi zikirusha video ya Diddy ikimuonesha anamshambulia aliyekuwa mpenzi wake Cassie iliyovunja miezi kadhaa iliyopita.

Mwanamuzi huyo alikamatwa Jumatatu, Septemba 16, 2024 na kushitakiwa kwa makosa matatu ulaghai wa kingono, usafirishaji wa binadamu ili kujihusisha na biashara hiyo ya ngono.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags