Mwanariadha wa kwanza kukimbia chini ya sekunde 10 afariki dunia

Mwanariadha wa kwanza kukimbia chini ya sekunde 10 afariki dunia

Mwanariadha kutoka nchini Marekani Jim Hines, mwanariadha wa kwanza kukimbia mbio za mita 100 chini ya sekunde 10, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76.

Alivunja rekodi hiyo mwaka wa 1968 aliporekodi sekunde 9.9 katika michuano ya Marekani. Hines pia akavunja rekodi yake mwenyewe muda mfupi baada ya kushinda dhahabu kwenye Olimpiki ya 1968, ambapo kipima muda cha kielektroniki huko Mexico City kilimrekodi kwa 9.95.

Rekodi yake ilidumu kwa karibu miaka 15 hadi Calvin Smith alipokimbia muda wa 9.93 mwaka wa 1983, Kifo chake kilitangazwa katika taarifa ya Riadha za Dunia, shirika hilo lilisema "limehuzunishwa sana" na habari hiyo.

Hines alizaliwa katika jimbo la Arkansas mnamo 1946 lakini alilelewa huko Oakland, California.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post