Mwanamitindo maarufu akutwa amefariki nchini Kenya

Mwanamitindo maarufu akutwa amefariki nchini Kenya

Polisi Nchini Kenya wanachunguza Chanzo cha mauaji baada ya kukuta mwili wa mwanamitindo maarufu Edwin Chiloba umetupwa Ukiwa Ndani ya Sanduku la Chuma.

Kulingana na chanzo kimoja cha habari ,mwendesha Bodaboda aliona gari ambalo halikuwa na namba likitupa sanduku la chuma kando ya barabara ya Kipenyo Kaptinga Nchini humo.

Kesi hiyo iliripotiwa kwa polisi wa Uasin Gishu ambao walifika eneo la tukio na walipofungua sanduku hilo, walikuta mwili wa mwanamume aliyekuwa amevalia nguo za kike uliokuwa ukianza ukioza.

Baadaye ilibainika kuwa marehemu alikuwa mbunifu wa mitindo wa Eldoret Edwin Chiloba.

Mwili huo ulipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Moi ukisubiri uchunguzi wa maiti kubaini chanzo cha kifo hicho.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags