Mwanamama aliyebadilisha ndege kuwa makazi

Mwanamama aliyebadilisha ndege kuwa makazi

Baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kuharibiwa na dhoruba la barafu mwanamama Jo Ann Ussery, maarufu 'Little Trump' ambaye alikuwa anajihusisha na masuala ya saluni aliamua kununua ndege kwa ajili ya makazi.

Wazo la kununua ndege hiyo lilikuja baada ya shemeji yake ambaye alikuwa muhudumu wa ndege ya Boeing 727 kumueleza kuhusiana na ndege hiyo kuuzwa kutokana na kuwa hitirafu ambayo haiwezi kurekebishika ndipo, Jo Ann aliamua kuinunua.

Kwa mujibu wa Daily mail Jo Ann alilipa dola 2,000 kwa ajili ya ndege hiyo na kutoa kiasi cha dola 4,000 ili kuitoa ndege hiyo na kuipeleka sehemu ambayo alitaka iwepo ambayo ni katika moja ya Ziwa huko Benoit.

Jo Ann alirekebisha ndege hiyo kwa kuweka vyumba vitatu vya kulala, kuunganisha umeme, mabomba ya maji, seble, sehemu ya kulia chakula, na kuweka bafu kubwa katika chumba cha marubani huku akigharimu zaidi ya dola 24,000.



Ndege hiyo, yenye nambari serial 19510, ilikuwa ndege ya kwanza ya Boeing 727 katika shirika la ndege la ‘Continental Airlines’ na ilikuwa ikihudumu kwa shirika hilo kuanzia Mei 1968 hadi Septemba 1993.

Jo Ann alihamia katika ndege aliyoibadirisha kuwa nyumba Aprili 1995 na kukaa huko hadi Mei 1999 alipofariki kwa ajali ya kuanguka na lori.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post