MWANA FA, WAKAZI, NAY WA MITEGO wamkalia kooni STEVE NYERERE

MWANA FA, WAKAZI, NAY WA MITEGO wamkalia kooni STEVE NYERERE

Wasanii wa muziki wa Bongo fleva wamemtaka msanii wa filamu nchini Steven Mengele maarufu Steve Nyerere ang’atuke kwenye uongozi ndani ya saa 48, kwa madai kuwa hawamtambui na hawako tayari kuwakilishwa naye.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Steve Nyerere kuteuliwa kama msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania (Shimuta).

Hata hivyo Steve Nyerere amekataa kuondoka kwenye nafasi hiyo liicha ya kupingwa na wasanii hao wa muziki pamoja na wadau mbalimbali wa muziki.

Akizungumza na waandishi wa habari Steve Nyerere amesema ikitokea akatenguliwa katika nafasi hiyo, Mahakama zipo.

Amesema hawezi kuachia nafasi hiyo kwa kuwa ana nia njema ya kuisadia tasnia ya muziki na kwamba wanaompinga ni kawaida yao kupinga mambo.

Kwenye Instagram yake Nay wa Mitego ameandika kwamba watu wasiichukulie kauli hiyo kama ubabe au utemi kwa kutumia nafasi yake kama Mbunge.

"Kauli ya Mwana Fa watu wasiichukulie kama kauli ya kibabe, kitemi na kutumia nafasi yake kama Mbunge lakini haya ni mawazo ya wasanii wengi ambao hawana nafasi ya kuongea na woga wakiamini Steve ni mtu wa ndani na ana-connection. wengi hatuungi mkono maamuzi ya shirikisho, na hiyo ni kauli yetu sio ya Mwana FA".

"Kama mtu hana sifa za uongozi tukikubali atuongoze ni kama tumekubali bora yaende. yasiwe masaa 48, yawe hata masaa 24. Steve tunakupenda kama msanii wa kuchekesha lakini sio msemaji na afisa mipango wetu".






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags