Mwakinyo abadilishiwa mpinzani, Kuzichapa na Mcongo

Mwakinyo abadilishiwa mpinzani, Kuzichapa na Mcongo

Bondia Hassan Mwakinyo Januari 27 atapambana ulingoni kuwania ubingwa wa WBO Afrika ambapo atapambana na bondia tofauti na yule aliyetangazwa awali Erick Msambudzi kutoka Zimbabwe.

Pambano hilo la raundi 10 la uzito wa kilo 72 litapigwa katika ukumbi wa ndani New Amaan Complex, Zanzibar na sasa Mwakinyo atazichapa na Mbiya Nkanku kutoka DR Congo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram bondia huyo ameandika ujumbe huo

"Ujumbe kwako Erick Msambudzi nasikitika Januari 27, 2024 New Aman Complex Indoor Zanzibar sitaweza kucheza nawe. Kwa sababu ya taratibu za wasimamizi wa ngumi duniani ingawa nilikupania na ulikuwa daraja moja jepesi kulivuka,"
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags