Musk aipinga Apple kutumia akili bandia

Musk aipinga Apple kutumia akili bandia

Mmiliki wa mtandao wa X zamani (Twitter) #ElonMusk amepinga kampuni ya Apple kutumia mfumo wa akili bandia (AI) kwenye iPhone na vifaa vyingine.

Musk ameweka wazi kuwa hakubaliani na matumizi hayo ya AI kwa sababu ni hatari kwa binaadamu na kuwataka watu kuchunguza vifaa vyao vya Apple kwa makini kabla ya kuvitumia.

Hayo yote ni baada ya kampuni ya Apple katika mkutano wa kila mwaka wa watengenezaji wa vifaa vya electronic uliofanyika mjini California, nchini Marekani kutangaza kuwa na mpango wa kuleta akili bandia kupitia vifaa vyao.

Ikumbukwe mwaka 2015 Musk alikuwa mwanzilishi wa OpenAI lakini ghafla aliachana na biashara hiyo na hivi karibuni ameitaja kuwa hatari kwa binaadamu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags