Museveni: Wabunge wapigwe marufuku kusafiri nje ya nchi

Museveni: Wabunge wapigwe marufuku kusafiri nje ya nchi

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametoa wito mwishoni mwa wiki wa kupiga marufuku safari za nje ya nchi kwa Wabunge na watumishi wa umma ili kuokoa fedha kwa mambo mengine yenye kipaumbele zaidi.

Museveni aliyasema hayo alipokuwa akituma vifaa katika taasisi ya Petroli ya Uganda-Kigumba (UPIK) ambapo nchi hiyo inatarajia kutoa mafunzo kwa wataalam wa ndani katika utafiti wa mafuta.

Uganda inatarajia kuanza kusukuma mamilioni ya mapipa ya mafuta mpaka ifikapo mwaka 2025 kutoka kwenye hifadhi yake kubwa ya mafuta, rais wan chi hiyo hakufurahishwa na kwamba taasisi ya mafunzo bado haijakamilika kutokana na ukosefu wa fedha.

"Waambie watumishi wa umma na wabunge waache kusafiri nje ya nchi, pesa zinapotea katika safari za nje na bado Kigumba inalilia pesa," alisema, kwa mujibu wa taarifa ya vyombo vya ndani.

Rais huyo pia alipendekeza kusimamishwa kwa posho zote, kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Daily Monitor.

Bomba la mafuta ghafi la $3.5bn (£2.7m) litakalounganisha maeneo ya mafuta ya Uganda mpaka bandari katika nchi jirani ya Tanzania limepingwa na wanaharakati wa hali ya hewa.

Licha ya kwamba nchi hizo mbili za Afrika Mashariki zinasema kipaumbele chao ni maendeleo ya kiuchumi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags