Museveni asimamisha kazi za waganga wa kienyeji

Museveni asimamisha kazi za waganga wa kienyeji

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameamuru waganga wa kienyeji kuacha kuwatibu watu, katika juhudi za kupambana na kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola. Watu 19 wamekwisha kufa kutokana na ebola katika mlipuko mpya wa ugonjwa huo, wa kwanza tangu mwaka 2019.

Aidha, Museveni amewaamuru maafisa wa usalama kuwakamata watu watakaokaidi kuwekwa karantini wanaposhukiwa kuwa na ebola. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya mkutano wa mawaziri wa afya wa nchi za kikanda kujadili hali ya mlipuko wa ebola.

Ambapo jana kulitolewa tamko na Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani, WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ameuarifu mkutano huo kwamba majaribio ya tiba dhidi ya aina ya Ebola inayosambaa Uganda yataanza mnamo wiki chache zijazo.

Visa 54 vya maambukizi ya ebola vimekwishathibitishwa nchini Uganda tangu kuripotiwa ugonjwa huo katika wilaya ya Mubende.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags