Museveni aonya mapenzi ya jinsia moja

Museveni aonya mapenzi ya jinsia moja

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amewaonya wananchi wake dhidi ya kampeni zinazounga mkono haki za wapenzi wa jinsia moja akieleza kuwa jambo hilo ni haramu nchini humo.

Mwaka 2014 ilisainiwa sheria ambayo inaruhusu kifungo cha maisha kwa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na ndoa za watu wa jinsia moja.

Siku ya Jumatano rais huyo alitaja haki za wapenzi wa jinsia moja kama ni upuuzi wakati wa hotuba aliyoitoa kwenye mahafali ya Chuo cha Kitaifa cha Ulinzi.

“Usilete upuuzi wowote hapa... Tulikuwa Washington, na wakati huu Wamarekani walipanga mkutano vizuri kwa sababu hawakuleta masuala haya. Walijikita kwenye biashara, suala ambalo ni zuri, hawakuleta masuala yeyote kuhusu wapenzi wa jinsia moja lakini kama wangeleta hizo mada tungekuwa na matatizo” alisema Museven

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post