Murphy mwigizaji bora wa kiume Oscar 2024

Murphy mwigizaji bora wa kiume Oscar 2024

Mwigizaji maarufu kutoka nchini Ireland, Cillian Murphy ameshinda Tuzo za Oscar 2024 katika kipengele cha Mwigizaji Bora wa Kiume, tuzo zilizotolewa usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa ‘Dolby Theatre’ uliopo California nchini Marekani.

Murphy amepata tuzo hiyo kupitia filamu ya #Oppenheimer, huku mwanadada Emma Stone akichukua Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike, akiwapiku Lily Gladstone, Annette Bening na Carey Mulligan.

Cillian Murphy ameonekana katika filamu mbalimbali zikiwemo ‘28 Days Later’, ‘The Delinquent Season’, ‘Red Eye’, ‘The Wind That Shakes the Barley’ na nyinginezo.

Mkali huyo wa ‘Oppenheimer’ amewahi kupokea tuzo nyingine kama ile ya ‘Academy’, ‘Golden Globe’, Tuzo ya BAFTA. Kwa upande wa tuzo za Oscar hii inakuwa ya kwanza kwake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags