Mume wa Simi afunguka kuwa na ugonjwa wa ‘Sickle Cell’

Mume wa Simi afunguka kuwa na ugonjwa wa ‘Sickle Cell’

Mume wa mwanamuziki kutoka nchini Nigeria #Simi, #AdekunleGold amefunguka kuwa na ugonjwa wa Sickle Cell ambapo ameweka wazi kuwa umekuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.

Tovuti ya CCN imeleza kuwa msanii huyo ameamua kuvunja ukimya na kupaza sauti juu ya ugonjwa huo kwani umekuwa ukichukua maisha ya watu wengi duniani.

 Ili kupambana na ugonjwa huo #AdekunleGold amedai kuwa nampango wa kuanzisha Taasisi iitwayo ‘Adekunle Gold Foundation’ itakayojihusisha na kusaidia watoto wanaopambana na ugonjwa wa #SickleCell Afrika nzima.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2022 Adekunle alitoa Wimbo wa ‘5Star’ ambapo ndani yake aliimba kuhusu Ugonjwa huo na jinsi unavyo athiri sana katika bara la Afrika.

Kwa mujibu wa shirika la Afya ulimwenguni linaeleza kuwa ugonjwa huo umeenea zaidi Afrika kwa kuchukua zaidi ya Asilimia 66 kutoka Duniani kote na huku nchi ya Nigeria ikiathiliwa zaidi ambapo watoto wapatao 150,000 huzaliwa na ugonjwa huo kila mwaka.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags