Mume ajiua kisa hajapikiwa kuku

Mume ajiua kisa hajapikiwa kuku

Mwanaume mmoja nchini Kenya, mwenye umri wa miaka 45 aliefahamika kwa jina la John Rugala, amefariki kwa kujiua baada ya Mke wake kuripotiwa kukataa kumpikia kuku akiwa nyumbani kwake Uriri, Kaunti ya Migori.

Msaidizi wa Mkuu wa Polisi wa eneo hilo, Nyaobe John Atonya amesema Mwanaume huyo alijifungia ndani ya nyumba yao kabla ya kujichoma moto, taarifa za awali zinaonesha kuwa Mkewe hakutaka kupika mboga hiyo kutokana na kuku huyo kuwa ni mali ya Binti yao.

Inadaiwa kabla ya kujiua John alimfukuza Mkewe nyumbani na baada ya tukio Wananchi walikimbilia eneo hilo kwa nia ya kuzima moto lakini juhudi zao zilifeli.

Aidha mwili wa marehemu umehamishiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Migori Level Four kusubiri uchunguzi huku Polisi wakitoa wito kwa wanandoa kutafuta njia mbadala za kutatua migogoro yao.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags