Muimbaji Marc Anthony afunga ndoa mara ya nne

Muimbaji Marc Anthony afunga ndoa mara ya nne

Muimbaji na muigizaji maarufu nchini Marekani, Marc Antony amefunga ndoa na mwanamitindo Nadia Ferreira, ambaye aliiwakilisha nchi ya Paraguay kwenye Miss Universe ya mwaka 2021. Inasemekana kuwa wawili hawa walifunga ndoa siku ya Jumamosi ya Januari 28, Florida.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, wawili hao walifunga ndoa kwenye jumba la Makumbusho la Sanaa la Pérez lililopo mjini Miami na kuhudhuriwa na watu mashuhuri akiwemo David Beckham na mkewe Victoria Beckham, muigizaji Salma Hayek, Maluma na Luis Fonsi na wengine.

Wanandoa hao walitangaza uhusiano wao kwa mara ya kwanza mwezi Machi 2022 na kutangaza kuchumbiana miezi miwili baadaye. Hii ni ndoa ya nne kwa Marc Anthony ambaye mwanzo aliwahi kumuoa Dayanara Torres kutoka 2000 mpaka 2004, Jennifer Lopez kutoka 2004 mpaka 2014, na Shannon De Lima kati ya 2014 hadi 2017.







Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags