Muandaaji wa Miss Rwanda ahukumiwa, Kwa unyanyasaji wa kingono

Muandaaji wa Miss Rwanda ahukumiwa, Kwa unyanyasaji wa kingono

Muandaaji wa miss Rwanda Dieudonne Ishimwe maarufu kama Prince Kid amefungwa miaka 5 kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono kwa mabinti wanaoshiriki mashindano hayo.

Hatua hiyo inakuja ikiwa imepita miezi 10 tangu mratibu huyo afutiwe mashitaka ya ubakaji na kuwaomba rushwa ya ngono washiriki wa shindano hilo.

Disemba 2022, hakimu alitoa hukumu ya awali dhidi ya Ishimwe inayoonesha hakuwa na hatia kutokana na upande wa mashitaka kukosa ushahidi wa kutosha na hivyo akaamuru aachiliwe.

Lakini hivi karibuni mambo yamekuwa tofauti kwake upande wa mashitaka ulikata rufaa ambayo uamuzi wake mpya umebaini alikuwa na hatia kutokana na ushahidi uliotolewa.

Waendesha mashtaka walitaka ahukumiwe kifungo cha miaka 16 jela, lakini jopo la majaji watatu limeamua atumikie kifungo cha miaka mitano kwa kuwa ni mara ya kwanza kwa mshtakiwa huyo kukutwa na uhalifu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags