Mtoto bilionea anavyoishi maisha ya kifahari

Mtoto bilionea anavyoishi maisha ya kifahari

Mtoto mwenye umri wa miaka 9 ni mmoja wa mabilionea mwenye umri mdogo zaidi duniani huku akimiliki nyumba yake binafsi na ndege.

Mtoto huyu ni mwana wa kiume wa mmiliki wa kampuni kubwa ya inteneti ya Nigeria Ismailia Mustafa, ambaye pia anafahamika kwa jina Momfa.

Mvulana huyu mwenye umri wa miaka 9-, kwa jina Mompha Junior, alipewa nyumba yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 6.

Mompha Junior, mara kwa mara hutuma picha zake nzuri kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram, akionyesha mtindo wake wa maisha ya kifahari.

Awali aliushirikisha umma picha ya ndege yake aina ya jet, ambapo akiandika “Usimdharau yeyote bure, na fanya kazi kwa bidii. Mungu awabariki watu.”

Baba yake Willkan Bw Mompha, ambaye ni meneja mkuu wa kituo cha kubadili pesa-Lagos Bureau De Change, anashutumiwa kwa ubadhilifu wa pesa wa zaidi ya Dola za Marekani Milioni 10.

Mapema mwezi huu, mahakama ya Nigeria ilisikiliza kesi iliyowasilishwa na tume ya Nigeria ya kupambana na ufisadi dhidi ya Ismail, iliyodai kuwa alikuwa amefanya ubadhilifu wa pesa kutoka katika biashara yake ya nyumba, ingawa Ismail anakanusha madai hayo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags