Mtoto amkata baba yake mdogo sehemu za siri, Njombe

Mtoto amkata baba yake mdogo sehemu za siri, Njombe

Polisi Mkoani Njombe wanamshikilia Grace Kiumbu mwenye umri wa miaka 30 Mkazi wa Kijiji cha Idindilimunyo Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe anayedaiwa kuwa ni Mgonjwa wa afya ya akili kwa tuhuma za kumjeruhi Baba yake mdogo Tiles Kiumbu mwenye umri wa miaka 60 kwa kuzikata sehemu zake za siri (uume) na kuziweka pembeni.

RPC wa Njombe Hamisi Issah amesema Mtuhumiwa Grace Kiumbu alimkata sehemu za siri Baba yake mdogo na kuitoa kabisa kwenye mwili wakati Baba yake akiwa amelala kwenye mkeka baada ya kulewa pombe.

“Wanasema huyu Grace ana tatizo ya ugonjwa wa akili lakini yeye anajieleza na anasema kuwa ‘Mimi ninatibiwa muda wote hapa (Kwa Baba yake anayedaiwa kuwa ni Mganga wa kienyeji) lakini safari hii nimekuja na nimetoa Tsh. Laki moja bila mafanikio huku naona watu wanaserebuka na kulewa pombe’, kwahiyo Baba yake alilala katika mkeka na huo ulikuwa urahisi wa Grace kufanya tukio hilo alimvua suruali na ndipo akamkata sehemu za siri” amesema RPC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags