Mtoto aliyempiga risasi mwalimu alitumia bastola ya mama yake

Mtoto aliyempiga risasi mwalimu alitumia bastola ya mama yake

Polisi nchini Marekani wamesema mtoto wa miaka sita alitumia bunduki ya mama yake iliyonunuliwa kihalali kumpiga risasi mwalimu wake katika shule moja nchini humo.

Katika mkutano na wanahabari siku ya Jumatatu, polisi huko Virginia walisema mtoto huyo alienda na bastola hiyo shuleni akiibeba kwenye begi lake la shule.

Polisi wanasema mtoto huyo alikusudia kumpiga risasi mwalimu wake na haikuwa bahati mbaya. Inaelezwa awali waligombana na mwalimu wake na mtoto huyo hakuridhika na kuchukua hatua hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags