Mtindo wa extension unavyobamba maharusi wengi

Mtindo wa extension unavyobamba maharusi wengi

Leo katika segment yetu ya fashion tutaelezea jinsi ya kutengeza nywele natural kwa kutumia mtindo wa extension hasa kwa mabibi harusi.

Urembo wa nywele ni moja kati ya jambo linalochukuwa nafasi kubwa katika muonekano wa mtu.

Kutokana na hilo kila kukicha kumekuwa kukibuniwa mitindo mbalimbali haswa kwa wanawake ili kuwawezesha kuboresha mionekano yao.

Siku za hivi karibuni kumeibuka mitindo mbalimbali ya nywele ilionekana kubamba katika maeneo mbalimbali.

Baadhi ya mitindo hiyo ni knotless ambao unataka kufanana sana na vibutu vya ‘rasta’, crochet pamoja na kufanya ‘extension’ haswaa tuta zungumzia namna mtindo huo unavyo pamba na kwenda na fashion.

Mtindo wa extension unataka kufanana sana na ule wa ushoneaji wa weaving tofauti yake kubwa ni huo unakupa muonekano unaoendana na nywele zako halisi yani mtu anapokutazama anaweza kudhani hizo ni nywele zako asilia.

Utofauti wa mtindo huo na ule wa ushonaji wa weaving ni extension hutumia kiasi kidogo cha weaving ambacho huchanganyikana na nywele halisia huku mtindo wa weaving kushonewa kichwa kizima.

Kwa sasa mtindo huo umekuwa ukitumiwa hata na baadhi ya maharusi ambao wanapenda kuonekana ‘natural’ katika siku hiyo muhimu.

Kupitia mtindo huo huwasaidia hata wale wanaoshindwa kumudu gharama za kununua wigi na wao kupata muonekano wa mzuri kupendeza wakiwa eneo la tukio na ngumu sana mtu kujua kama sio nywele zako kulingana na zitakavyo tengenezwa vizuri.

Ukipita katika kurasa za mitandao ya kijamii utaweza kuona ‘saluni’ mbalimbali utaona mtindo huo unasukwa kwa gharama ya kuanzia Sh35, 000 hadi 100,000 wengine gharama zao zikijumuisha na weaving au la kwa mantiki hiyo inaonyesha mtindo huo si wa gharama sana ila ni mzuri kwa sababu unakupa muonekano wa pekee.

Mwananchi Scoop ilipata wasaa wa kuzungumza na mtaalam wa masuala ya urembo wa wanawake kutoka katika ‘saluni’ ya Goddess Glam Beauty, Precious Simba yeye anatueleza mtindo huo hautumiki kwa ma-bibi harusi tu pekee bali huweza kutumika kwa mtu yeyote anaependelea kuwa namuonekano wa nywele ndefu bila kuvaa ‘wigi’ anasema.

“Pamoja na sherehe lakini pia mtindo huo wa nywele mtu anaweza kuutengeneza kwa ajili ya kwenda katika mikutano au kazini na shughuli zinginezo,”alisema Precious.

Anaendelea kueleza mtindo wa ‘extension’unaweza kutengenezwa kwa kushonea au ku-bond ‘weaving’ au kusukia katikati ya nywele halisi aina ya nywele bandia au uzi unaofanana na nywele halisi.

Precious amesema ili kupata muonekano mzuri unapotaka kufanya ‘extention’ ni vyema kuzingatia uchaguzi mzuri wa weaving ambalo linaendana sambamba na nywele yako halisi na inaruhisu kupasika na pasi ya nywele ili kuweza kunyoosha, kuweka mawimbi na mitindo mingine mbalimbali.

“Rangi ya nywele yako inapendeza zaidi ikifanana na ile ya rangi ya ‘weaving’ ili muonekano wake uje kuwa kama wa nywele halisia,”alisema.

Pia aliongezea kuwa ni muhimu kuhakikisha nywele za muhusika zina dawa ndefu sana au wastani lakini pia zenye afya ili zinapochanganywa na weaving iwe inavutia.

Mimi tu nikwambie mwisho wa week hii ndio mwanzo wa week nyengine tukutane tena hapa hapa Mwananchi Scoop tuweze kukujuza mengi zaidi kuhusiana na fashion.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags