Msongo wa mawazo unavyoweza kukusababishia matatizo ya kiafya

Msongo wa mawazo unavyoweza kukusababishia matatizo ya kiafya

Mark Lewis

Msongo wa mawazo ni mfadhaiko wa akili anaoupata mtu kutokana na shida, taabu, dhiki, matatizo au changamoto zinazomkabili katika maisha ya kila siku.

Mtu hupata msongo wa mawazo pale anaposhindwa au kukosa namna ya kukabiliana na jambo linalomsumbua.

DALILI ZA MSONGO WA MAWAZO.

Sisi sote tunapitia msongo wa mawazo kwa njia tofauti. Mara nyingi, tunaweza kosa kujua kuwa tunachopitia ni msongo wa mawazo. Ikiwa unapata mabadiliko haya, kuna uwezekano kuwa unakabiliwa na msongo wa mawazo.

  • Kupoteza hamu na tamaa ya kufanya uliyofurahiya hapo awali
  • Kuhisi kushuka moyo, au kukosa ttumain
  • Kuhisi vibaya kujihusu, au kuhisi kuwa umefelu maishani ama kwamba umeiangusha familia yako.
  • Kujisikia uvivu au kuhisi kutotulia, kubabaika.
  • Mawazo kwamba ungekuwa bora kufa au kujiumiza kwa njia fulani.

VISABABISHI VYA MSONGO WA MAWAZO

 Kuna vitu vingi vya kimazingira au kimsukumo vinavyoweza kusababisha uwe na msongo wa mawazo, vitu hivi hutwa “stressors”.

Stressor ni kitu cho chote kinachodai matumizi ya juu ya uwezo na nguvu zako za mwili. Inawezekana kuwa kikawa kitu kizuri tu, kama kuoa/kuolewa, kununua nyumba, kujiandaa kwenda chuoni au hata kupandishwa cheo kazini.

Vitu ambavyo vinasababisha msongo wa mawazo ni pamoj na:

 -Mabadiliko ya maisha au shule

- Matatizo katika mahusiano

- Matatizo ya kifedha

- Kubanwa na shughuli nyingi

- Watoto na familia

- Wasiwasi wa muda mrefu

- Tabia ya kuona kila kitu ni kibaya

- Kupenda yasiyowezekana

- Kutaka kila kitu kiwe sahihi (kikae juu ya mstari) kila wakati

- Kutopenda kushauriwa au kubadilika kutokana na hali halisi

- Kujidharau mwenyewe kwenye mazungumzo.

NAMNA YA KUDHIBITI MSONGO WA MAWAZO.

Licha ya msongo wa mawazo kuwa kitu cha kawaida maishani mwetu, inaweza kuwa hatari isiposimamiwa vizuri.

Usiruhusu hisia zinazohusiana na mafadhaiko na msongo wa mawazo zidhibiti maisha yako. Ikiwa unahisi kusumbuka na kuzidiwa, unashauriwa kufanya:

  1. Mazoezi

Shughuli kama vile kukimbia, kucheza mpira wa miguu, kutembea, na kucheza, kati ya

Zingine zitasaidia kuinua mhemko wako na kukusaidia kulala vizuri. Kufanya mazoezi mara kwa mara pia hukusaidia kusahau wasiwasi na shida zako na husaidia kusahau

  1. Kulala

Kulala hupunguza msongo wa mawazo sana. Kuwa na utaratibu wa kulala husaidia kukutuliza, inaboresha hali yako na nakusaidia kufanya maamuzi bora.

Wataalamu wa afya wanapendekeza kulala kwa angalau masaa 8 kila usiku.

  1. Lishe Bora

 lishe bora inaweza kuongeza mhemko wako, kupunguza shida za kuwa na shinikizo la damu, na kujenga kinga yako ya mwili. Kuna vyakula ambavyo vinaweza kupa utulivu wa msongo ikiwa unazijumuisha kwenye lishe yako ya kila siku. Hii ni pamoja na vyakula vyenye:

Vitamini C na madini - matunda na mboga

  • Protini kama mayai, nyama, na maharagwe.
  • Vyakula vinavyotoa nishati kama mahindi, ngano na viazi vitamu.
  1. Panga kazi yako na uorodheshe majukumu yako.

Panga kazi zako za kila siku ukianza na kazi za haraka. Mwishoni mwa siku, zingatia majukumu ambayo umeweza kufanya. Hii itakusaidia kukumbana na hisia za kuzidiwa na shughuli zako za kila siku.

  1. Zungumza na watu unaowaamini. Kuzungumza na kuwaambia watu wa karibu nawe shida zako kunaweza kusaidia kupunguza viwango vyako vya msongo wa mawazo, huku kujumuika na familia na marafiki kukiweza kukusaidia kuwa mtulivu na kupunguza msongo wa mawazo. Ni vizuri kuzungumza na wengine kwani watu wanaweza kukusaidia kupata suluhisho la kile kinachokusumbua. Kumbuka, kuna watu ambao wanaweza kuwa wamepitia hali kama wewe.
  2. Epuka njia mbaya za kukabiliana na msongo wa mawazo. Njia hizo ni pamoja na:-
  • Kuvuta sigara
  • Kunywa pombe sana
  • Kula sana au kula kidogo
  • Kukaa kwenye TV au kompyuta, saa nyingi sana
  • Kujitenga na marafiki, familia na shughuli
  • Kutumia vidonge
  • Kulala sana
  • Kuahirisha mambo
  • Kujishughulisha saa zote kuepuka matatizo
  • Kuwatulia wengine msongo wao (kubwatuka, kufoka, kupigana) 
  1. Tafuta huduma za ushauri wa kitaalamu.

Unapaswa kutafuta msaada ikiwa una mawazo ya kujiumiza, kuhisi kuzidiwa, kuhisi kuwa huwezi kukabiliana na tatizo lako.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags