Mshukiwa wa mauaji ya Tupac anyimwa dhamana

Mshukiwa wa mauaji ya Tupac anyimwa dhamana

Jaji wa Mahakama ya Wilaya ya Clark, Carli Kierny amemnyima tena dhamana Duane “Keffe D” Davis, mshukiwa wa mauaji ya marehemu mwanamuziki Tupac Shakur, mauaji yaliyotokea mwaka 1996 huko Los Angeles.

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Boston Globe’ imeeleza kuwa Keffe D ameomba dhamana hiyo ili aweze kwenda kupatiwa matibabu lakini mahakama hiyo imekuwa ikimkatalia dhamana mara kwa mara toka alivyokamata Septemba 2023.

Aidha jaji wa mahakama hiyo Carli Kierny ameweka wazi kuwa sababu ya kutokupokea dhamana hiyo inayogharimu dola 750,000 ni kutokana na kuwa na hisia mbaya zinazojaribu kufichwa na mtoaji wa dhamana hiyo ambaye ni "Wack 100".

Hata hivyo Davis amekana mashtaka ya mauaji ya daraja la kwanza. Pia siku ya Jumanne, jaji Kierny alisogeza tarehe ya kuanza kwa kesi hiyo tena kutoka Novemba 4, 2024 hadi Machi 17 mwakani.

Tupac Shakur alifariki Septemba 7, 1996, baada ya kupigwa risasi akiwa kwenye gari huko Las Vegas, Nevada.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post