Mshtakiwa wa mauaji ya kimbari afikishwa mahakamani

Mshtakiwa wa mauaji ya kimbari afikishwa mahakamani

Mmoja wa washtakiwa wa mwisho waliokuwa wanasakwa kwa kuhusika kwao katika mauaji ya kimbari Fulgence Kayishema, mwaka 1994 nchini Rwanda, amefikishwa mahakamani mjini Cape Town nchini Afrika Kusini siku mbili baada ya kukamatwa.

Kayishema ambaye alikuwa mafichoni kwa kipindi cha miaka 22, anakabiliwa na mashtaka hayo ikiwemo mauaji ya kimbari na njama ya mauaji hayo yanahusisha watu 2,000 kutoka kabila la Watusti nchini Rwanda.

Mwendesha mashtaka wa serikali Afrika  Kusini Eric Ntabazalila  amesema wali aliiambia shirika la habari AFP kwamba Kayishema atafikishwa mahakamani leo Ijumaa.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post