Mr P atuma barua ya wazi kwa Rudeboy

Mr P atuma barua ya wazi kwa Rudeboy

Nyota wa muziki Nigeria, Peter Okoye ‘Mr P’ wa kundi maarufu la muziki la ‘Psquare’ ameandika barua ya wazi kwa pacha wake Paul Okoye ‘Rudeboy’.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Mr P, alimtaka pacha wake afahamu kuwa hakuwa kwenye ushindani na yeye wala na mtu yoyote yule hivyo kuendelea kufanya mahojiano ya kumdhalilisha kwenye mitandano ya kijamii hakutomsaidia chochote.

Aidha mwanamuziki huyo alifunguka zaidi akiweka wazi kuchukizwa na Rudeboy kutangaza kuwa yeye ndio alikuwa akihusika kutunga nyimbo na kufanya project nyingine katika kundi hilo kwa asilimia 99.

Mbali na hayo kupitia barua hiyo ya wazi pia ameeleza juu ya pacha wake huyo kumkosea heshima mke wake, kipaji chake pamoja na familia yake kwa ujumla.



Ikumbukwe kuwa Agosti 2, 2024 Paul Nonso Okoye ‘Rudeboy’ alithibitisha kuwa kundi la #PSquare limegawanyika kwa mara nyingine kwa kudai kuwa toka walivyoungana hakuna cha maana kilichowahi kufanyika.

Kundi P-Square lilisambaratika kwa mara ya kwanza mwaka 2016 na kuungana tena mwaka 2021, huku mwishoni mwa mwaka jana kukiwa na tetesi kuwa wawili hao wamegawanyika tena.

Wawili hao walitamba na ngoma zao kama ‘Taste The Money (Testimony)’, ‘Personally’, ‘Forever’ pia wamewahi kutoa kolabo na mwanamuziki #Diamond wimbo uitwao ‘Kidogo’






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags