Mr Blue: Marafiki waliniharibu

Mr Blue: Marafiki waliniharibu

Mwanamuziki Mr Blue ameweka wazi kuhusiana na safari yake ya muziki ambapo amedai kuwa yeye aliharibiwa na watu (marafiki) ambao walikuja baada ya yeye kuwa ‘staa;.

Mr Blue ameyasema hayo katika mahojiano yake na BBC ambapo alifunguka kuwa kuna kipindi alipotea kwenye muziki kutokana ana kufuata starehe na marafiki wabaya.

“Mimi wakati naanza muziki nilikuwa mtoto na sikuwa na rafiki hata mmoja lakini watu walikuja wakijifanya wananijua wamesoma na mimi kwahiyo ule ushkaji mtu akivuta na mimi navuta mara pombe nikawa siendi studio, Mimi nimeharibiwa na watu waliokuja baada ya mimi kuwa Staa”

Hata hivyo alitoa shukrani kwa mkewe kwani ndiye mtu pekee ambaye alichangia kwa kiasi kikubwa cha yeye kubadirika kutoka katika makundi mabaya na kurudi katika game ya muziki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags