Wakati shughuli za uapisho wa Rais mpya wa Marekani Donald Trump zikifanyika jana Januari 20,2025. Mke wa Rais huyo Melania Trump alitokea kwenye hafla hiyo akiwa amevalia sketi ya penseli na koti refu lenye rangi nyeusi ambalo alivalia kwa juu, huku kichwani akiwa na kofia pana.
Kofia hiyo ambayo ilichukua nafasi yake kwenye uapisho huo, ilibuniwa na mbunifu wa mavazi Eric Javits ilionekana kulinda macho ya mwanamama huyo.
Kupitia mahojiano aliyofanya na ABC news mbunifu wa kofia hiyo amesema kumvalisha mke wa Rais ambaye ndiye mwanamke wa kwanza nchini humo, imekuwa moja ya heshima kubwa katika kazi yake.
"Wigo wangu wa sanaa ulinipa makali katika kuleta maelewano na usawa wa uso kwa kuunda maumbo ya kofia ambayo yangependeza na kuimarisha sura yake. Katika kazi hii mahususi ambayo haikuwa ngumu kufanyika kwa kuwa Melania Trump amebarikiwa na muundo mzuri, urembo na hali ya ajabu ya mtindo," amesema Eric
Kofia hiyo ilijidhihirisha wakati wote wa uapisho huo hususani wakati Trump akimbusu mkewe ambapo kofia iliacha nafasi hadi kupelekea Rais aliyepita Joe Biden kuizungumzia.
Hata hivyo mbunifu wa kofia hiyo Eric aliomgezea kuwa wakati akiitengeneza aliiona ya kawaida.
"Nilipokuwa nikiunda kofia mikononi mwangu ilikuwa rahisi. Ilikuwa ya kawaida lakini nilipoiona juu ya kichwa chake, ilibadilika sana. Hivyo ilikuwa sanaa nzuri na yenye nguvu bila shaka ninashukuru sana kwa kuorodheshwa kumtengenezea hilo,"
Leave a Reply