Mke wa Biden aanza ziara yake nchini Kenya na Namibia

Mke wa Biden aanza ziara yake nchini Kenya na Namibia

Mke wa Rais wa Marekani Jill Biden anatarajiwa kufanya Ziara nchini Namibia na Kenya siku ya Jumatano anapoanza ziara yake ya siku tano barani Afrika.

Ikulu ya White House ilisema ziara hiyo itakuza ushirikiano wa Marekani na barani Afrika na vipaumbele vya pande zote kwa bara hilo. Jill Biden ni afisa wa tano wa ngazi ya juu wa Marekani kutembelea bara hilo

Aidha Waziri wa Biashara wa Marekani Janet Yellen, Balozi katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Masuala ya Afrika Molly Phee na mwakilishi wa viongozi wa Marekani na Afrika Johnnie Carson ni maafisa wengine wakuu ambao wamezuru bara hilo tangu kumalizika kwa mkutano huo.

Wachambuzi wanasema mtazamo mpya wa Marekani kwa Afrika ni jaribio la kukabiliana na ushawishi wa China na Urusi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags