Mfalme wa Pop kutoka Marekani Michael Jackson ameripotiwa kuacha deni la dola 500 milioni ikiwa ni sawa na Sh 1.3 Trilioni Mahakama Kuu ya Kaunti ya Los Angeles imesema.
Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Nbs News’ imeeleza kuwa wakati MJ anafariki mwaka 2009 aliacha deni litokanalo na ziara yake ya ‘This Is It’ ambapo alikopa pesa ili kufanikisha show hiyo iliyopangwa kuoneshwa zaidi ya mara 50 katika ukumbi wa ‘O2 Arena’ jijini London.
“Wakati wa kifo cha Michael Jackson, aliacha deni linalogharimu dola milioni 500, na mpaka kufikia sasa deni hilo limeshakuwa na viwango vya juu vya riba, pamoja na deni jingine la dola milioni 40 analodiwa na promota wa watalii, AEG” imesema taarifa kutoka mahakamani.
Aidha kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mahakama imewataka watunzaji wa mali za Michael Jackson kulipa deni hilo kabla ya riba haijaongezeka zaidi.
Michael Jackson ‘MJ’ alizaliwa August 29, 1958, Gary, Indiana, Marekani na kufariki June 25, 2009 akiwa na umri wa miaka 50 huku akiacha tuzo 13 za Grammy pamoja na rekodi ya mauzo ya kazi zake yaliyogharimu dola 400 milioni.
Leave a Reply