Mixtape ya marehemu Rich Homie yashika namba  1 Apple Music

Mixtape ya marehemu Rich Homie yashika namba 1 Apple Music

Mixtape ya marehemu mkali wa Hip Hop kutoka Marekani Rich Homie Quan iitwayo ‘I Promise I Will Never Stop Going In’ imeripotiwa kushika namba moja kwenye mtandao wa kusikiliza muziki wa ‘Apple Music’ nchini humo.

Mafanikio haya yanakuja ikiwa ni siku mbili tuu zimepita tangu kutangazwa kwa kifo cha msanii huyo ambapo kwa mujibu wa tovuti mbalimbali Marekani zimeweka wazi kuwa muziki wa Rich umepata mashabiki wapya ambao wamepelekea Mixtape hiyo kushika nafasi ya kwanza katika mitandao kadhaa ya kusikiliza na kupakua muziki.

Ikumbukwe kuwa Mixtape hiyo iliachiwa Novemba 26, 2013 ikiwa na nyimbo 17 zikiwemo ‘Cash Money’, ‘They Don't Know’ na nyinginezo.

Mixtape ni mchanganyiko wa nyimbo ambazo msanii wa Hip Hop anaziachia, na mara nyingi hupatikana kwa bei rahisi au bure ambapo msanii anaamua kufanya hivyo kwa lengo la kujiweka karibu na mashabiki zake.

Rapa Rich Homie Quan (34) amefariki dunia akiwa nyumbani kwake jijini Atlanta Marekani siku ya jana Alhamisi Septemba 5, 2024 huku sababu ya kifo chake ikidaiwa kuwa ni kuzidisha dawa za kulevya.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags