Miwani kwa Tiwa siyo fashion, ni matatizo

Miwani kwa Tiwa siyo fashion, ni matatizo

Baada ya baadhi ya mashabiki kudadisi kuhusiana na uvaaji wa miwani kwa mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Tiwa Savage, hatimaye mwanamuziki huyo ametoa sababu ya kwanini huvaaa miwani muda wote ambapo ameeleza kuwa amekutwa na tatizo la macho.

Tiwa kupitia Instastrory yake ameweka wazi suala hilo kwa kudai kuwa miaka miwili iliyopita alipata shida ya kutooni vizuri ‘uoni hafifu’ katika kusoma, vitabu na Sms zinanazoingia katika simu yake, ndipo Daktari wake akamshauri kutumia miwani muda wote, kutokana na hali kuwa mbaya zaidi katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags