Miss World kufanyika India

Miss World kufanyika India

Wakati Miss Tanzania wakiendelea kujichua na mashindano, hatimae waandaaji wa mashindano ya ulimbendwe Duniani (Miss World) wameweka wazi fainali za mwaka huu zitafanyika Desemba 9 nchini India.

Tanzania itawakilishwa na Halima Kopwe, miss Tanzania mwaka 2022. Nikurudishe nyuma kidogo katika moja ya mahojiano ya mrembo huyo aliyofanya na Mwananchi alieleza namna alivyojipanga kufanya vizuri hasa kwenye kinyang'anyiro cha mataji madogo madogo katika fainali hizo.

“Naendelea kufanya project yangu ambayo nitakwenda nayo kwenye Miss World, sijajua ni lini na wapi zitafanyika, lakini niko vizuri na naamini nitafanya vizuri zaidi kwenye yale mataji madogo madogo ambayo yatanisogeza kwenye nafasi ya kufanya vizuri” alisema Halima alivyohojiwa na Mwananchi miezi michache iliyopita.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags