Miss Rwanda atupwa gerezani

Miss Rwanda atupwa gerezani

Baada ya kukutwa na hatia ya makosa matatu ya kuendesha gari bila leseni, akiwa amelewa na kukimbia eneo la tukio baada ya ajali iliyoharibu miundombinu, mshindi wa taji la Miss Rwanda mwaka 2022 Divine Nshuti Muheto amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na miezi nane.

Divine alifikishwa Mahakamani Alhamisi jana Oktoba 31, 2024 na kuhukumiwa kifungo hicho ambacho kimegawanyishwa kwa makosa yake matatu ambayo ni miezi 6 kwa kuendesha akiwa amelewa, miezi miwili kwa kuendesha bila leseni na mwaka mmoja kwa kukimbia eneo la tukio baada ya kusababisha ajali na kuharibu miundombinu.

“Alikuwa na kiwango cha kilevi hadi point 4 huku kiwango kinachokubaliwa mi kipimo cha point 0.8”

Hata hivyo Hakimu wa Mahakama hiyo baada ya kusikiliza pande zote mbili amesema hukumu rasmi itatolewa November 6, 2024 huku Miss huyo akiendelea kushikiliwa na Polisi.

Aidha kwa upande wa Divine alikili makossa mawili likiwemo la kuendesha akiwa amelewa na kuendesha bila leseni lakini aliweka wazi kuwa hakukimbia kwa lengo la kutoroka alikimbia baada ya wakazi wa eneo hilo kukusanyika kwa wingi hivyo alihofia kujeruhiwa.


Divine Nshuti Muheto alipata umaarufu baada ya kuondoka na taji la shindano la Miss Rwanda mwaka 2022 kabla ya shindano hilo kusitishwa na Serikali nchini humo kwa tuhuma za maadili mabovu kwa waandaaji wa shindano hilo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags