Misingi waliyowekeana Paula na Marioo

Misingi waliyowekeana Paula na Marioo

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Marioo amesema yeye na mzazi mwenzie Paula Paul ni watu wanaoaminia ndiyo maana hawashikiani simu.

"Sisi Gen-Z tunapenda maandiko kwamba usishike simu ya mpenzi wako kama unataka ndoa yako ifanikiwe, na sisi tunaaminiana. Vipo vitu tulishaongea kwamba ikifika hatua hii mimi na wewe basi kwa hiyo naamini amesikia, ameheshimu na anaogopa hawezi kufanya tofauti ndiyo maana siwezi kushika simu yake,"amesema kwenye mahojiano yake na Clouds Media

Marioo amesema licha ya kutochunguza simu ya Paula lakini ana mitandao mbalimbali ya kijamii ya Paula kwenye simu yake.

Kwa upande wake Paula amesema hayupo tayari kujua nywila za Marioo za simu yake

"Sitaki kuwa na password ya simu ya Marioo, kila mtu ana simu yake,"amesema Paula

Hata hivyo Paula amesema kabla ya Marioo kufanya video yeye ndiye humchagulia wanawake wa kufanya nao video za nyimbo zao.

"Kabla hajashuti na mwanamke huwa najua, kuna wakati namtafutia, huwa naangalia vigezo awe mwanamke mrembo na shepu kwenye video awe anavutia. Namuamini najua hawezi kufanya chochote,"amesema Paula kwenye mahojiano hayo






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags