Miili 236 iliyoko sehemu ya kuhifadhia maiti nchini Kenya kutupwa

Miili 236 iliyoko sehemu ya kuhifadhia maiti nchini Kenya kutupwa

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na chombo cha habari cha Citizen TV Kenya kimeeleza kwamba miili ya watu waliofariki dunia itatupwa hivi karibuni. Miili hiyo iko katika vyumba vya kuhifadhia maiti vya Jijini Nairobi toka Machi 2021 mpaka Machi 2022.

Wananchi wametakiwa kwenda kuitambua miili hiyo na kuichukua na endapo haitatambuliwa au kuchukuliwa ndani ya Siku 7, kaunti ya Nairobi itaitupa miili hiyo.

Aidha walielezea kuhusiana na sababu za Vifo vya marehemu hao ambapo ni ajali za barabarani, mauaji, kuzama majini, kupigwa risasi, Kifo cha kawaida na kifo cha ghafla, ambapo baadhi ya miili hiyo imetambuliwa kwa majina, huku mingine ikiwa haijajulikana.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post