Michezo bora kwa vijana hii hapa

Michezo bora kwa vijana hii hapa

Games are a part of making someone to have fun at a certain moment, do you appreciate this young ladies and gentlemen? Let’s say something unique kwenye masuala ya michezo kwa vijana, imekaaje hiyo mtu wangu?.

Haswaaa!!  Michezo sikuzote hutuweka huru na kutufanya tujisikie furaha na amani wakati wote si hivyo tu! Lakini pia games ni sehemu moja wapo ya kujenga miili yetu, afya na akili pia.

Nani anapinga kwenye hili? Ukiwa mpizani hapa basi wewe utakua sio mwanachama wa michezo, hivyo huwenda usielewe nini namaanisha hapa lakini kwa wale wakali wa hizi kazi tunafahamiana vizuri kabisaa hapa!

Yeees!!! vijana wengi hupenda kujishughulisha na michezo mbalimbali Kulingana na mtu mwenyewe ni mchezo gani anaoukubali lakini je, unafahamu ni namna gani michezo hutujenga zaidi kifikra na kimtazamo?.

Makala hii italenga moja kwa moja katika kuangazia michezo bora hususani kwa vijana, umewahi kufikiria kuwa michezo ina nafasi kiasi gani kwa kijana? Basi fuatilia makala hii.

Mchezo wa kwanza ninaoanza nao hapa ni huu hapa chini, wenyewe wakali wa hizi kazi wanaulewa vilivyoo hasaa kitu hiki hapaaaa!

  • Cricket

Huu ni mchezo bora zaidi kwa  vijana, na una mashabiki zaidi ya bilioni 3 huko Ughaibuni ikiwemo Australia, Uingereza na Asia na  duniani kote.

Mchezo huu husaidia zaidi ukuaji kamili kwa vijana, chukua hiyo ifanyie kazi mwanangu mwenyewe.

  • Mpira wa Miguu

Soka ni moja kati ya mchezo maarufu sana duniani inayochezwa na vijana wengi pamoja na mashabiki wengi, pia soka ni moja wapo ya  michezo(3) bora Ulimwenguni.

Ukiwa unaongozwa na nchi zaidi ya 208 ukichezwa mchezo huo.

  • Mpira wa wavu

Huu nao sio wakukosa kabisa, mara nyingi mchezo huu vijana wenye afya  huupambania sana na huwa hodari na wepesi,  mpira wa wavu kama michezo mingine ya timu inayohusiana na huu.

Ni rahisi sana kama ilivyo michezo mingine na ni  bora sana kwa vijana kucheza, volleyball inahusisha mwili wa juu, mikono, mapaja na miguu ya chini, unasaidia kuboresha usawa wa mwili na fikra.

Kwenye mchezo huu vijana hujifunza mengi sana ikiwemo mawasiliano na kufanya kazi kwa pamoja as a team.

  • Mazoezi kwa viungo

Vijana wengi wanajihusisha na harakati za mazoezi siku hizi wakati wa Olimpiki utashuhudia maajabu mengi sana, unaweza ukawa sio mchezo rahisi kama ilivyo mengine lakini vijana huupenda sana.

Vile vile ili kuzuia ugumu wa mwili, mazoezi ya viungo yanashauriwa kwa vijana ili kubadilika kwa mwili kwa ujumla kunaweza kuletwa na mazoezi ya viungo.

  • Baseball

Mchezo huu ulianza tangu mnamo mwaka 1876, vijana wengi huko Japan wanaufurahia mchezo huu, huu ni mchezo unaoendeshwa na America ukiwa na mashabiki takriban milioni 500.

Ligi muhimu zaidi za baseball duniani ni ligi ya Nippon na MLB ambazo zinamilikiwa na Japan na mtawala wake America.

Mchezo huu unahusisha harakati nyingi zinazofaidisha vijana kwa njia nyingi pamoja na shughuli kama vile kutupa mpira, kuzungusha gongo, kukimbia kwa besi mara nyingi mchezaji huwa akihama akijaribu kushinda michezo kwa timu yake.

Kama mchezo mwengine wowote ambao unajumuisha harakati nyingi baseball husaidia kujenga uvumilivu, kuongeza utendaji wa moyo na kupunguza hatari ya kunenepa sana.

  • Tennis

Kama kawaida mchezo huu nao hukubalika sana kwa vijana kama mchezo wa kibinafsi tennis huweka kila mchezaji kando na kuruhusu kila mtu kupambana kwa kasi yake mwenyewe.

Kutokana na muda mrefu uliotumika kucheza seti, tennis huwapa vijana uwezo wa kukuza uvumilivu, utaratibu wa mwil, macho na kasi.

Mfano wa vijana wanaocheza mchezo huu Rodger Federer, Raphael Nadal, Novak Djkovic, Serena William.

Naaam! Hiyo ndo michezo inayofukuziwa na vijana wengi ulimwenguni lakini je unajua faida za michezo kwa vijana? Hata usiende mbali leo tunamaliza kila kitu hapa.

Michezo inaruhusu vijana kushiriki katika shughuli nyingi za mwili kama vile kukimbia, kuruka, na kupiga mbizi,

Kuboresha ujuzi wa kutatua changamoto

Kila mchezo wa mashindano kwa njia isiyo ya moja kwa moja hufundisha jinsi ya kushinda Changamoto, vijana ambao hucheza michezo hukaribia kila changamoto ma hali ya akili kutafuta njia za kushinda changamoto hizo.

 Kuboresha Afya zaidi

Mazoezi ya kawaida ni moja ya funguo za maisha bora, michezo husaidia vijana kupunguza hatari ya kuathirika na magonjwa Fulani wakati wa uzee.

Eeebwana eeeeh hii ndio michezo bora inayopambania na vijana wengi kwa sasa ulimwenguni tambua kuwa michezo siku zote itakufanya uwe bora na imara zaidi.

Halkadhalika usisahau hii michezo hujenga watu kimtazamo, kifikra hata kimwil,i kupitia michezo kuna mengi sana yakujifunza na kwenda nayo sawaa ama nini?.

Wewe unaonaje hili, unakubaliana na concept hii? Tuambie kupitia ukurasa wetu wa Instagram @mwananchiscoop, toa maoni yako. Wishing you a happy furahi day,  enjoy your wikieeendii!!!!!!

.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags