Mhubiri mwenye watoto 289 kuhojiwa na polisi

Mhubiri mwenye watoto 289 kuhojiwa na polisi

Mhubiri Ronald Wanyama, anayejulikana pia kama Nabii Yohana raia wa Kenya, ametakiwa kufika mbele ya Kamanda wa Polisi wa Bungoma, Juni 2, 2023 kwa ajili ya kujieleza.

Mhubiri huyo mwenye umri wa miaka 83 anayeendesha kanisa la Church for All Nations huko Kanduyi, Bungoma amewahi kuvuma hapo awali kwa madai ya kuzindua biblia yake mwenyewe na sarafu yake.

Kwa mujibu wa Franci Kooli, Kamanda wa Polisi Kaunti ya Bungoma, mhubiri huyo atahojiwa kuhusu jinsi kanisa lake linavyofanya kazi, Mtandao wa Tuko umeripoti.

Kooli alisema kuwa mhubiri huyo ambaye ana wake 42 na watoto 289 anachunguzwa kwa madai ya mafundisho yenye utata.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags