Mfumo unamgharimu kuwika kimataifa

Mfumo unamgharimu kuwika kimataifa

Wameingia kwenye mfumo!. Ni kauli aliyoitoa staa wa Bongofleva, Diamond Platnumz baada ya wimbo wake ‘Komasava’ kubamba sehemu nyingi duniani ikiwemo Nigeria ambapo wasanii wake wamekuwa wakifanya vizuri kwa miaka.

Kwa mujibu wa Diamond, tasnia ya muziki Nigeria imekuwa haimpi heshima anayostahili kutokana na ukubwa wa jina lake Afrika, ila sasa kwa jinsi Komasava inafanya vizuri wenyewe wamejikuta wakikubali yaishe.

Hata hivyo, ukweli ni kwamba kuna eneo moja ambalo linamtofautisha Diamond na washindani wake kimuziki Afrika hasa kutokea Nigeria kama vile Davido na Burna Boy ambao wamewahi kufanya nao kazi miaka ya nyuma.

Nalo ni namna ambavyo wanaandaa kazi zao, kuzitoa na walengwa hasa wa kazi hizo, katika eneo hilo, Diamond amebeba mzigo mkubwa ukilinganisha na wenzake na hapo ndipo wanamzidi kimauzo na hata shoo za kimataifa. Kivipi?

Katika ujumbe wake wa Januari 21, 2023, Diamond alitangaza kuwa mwaka huo angefanya mambo makubwa katika muziki kama ndiyo ametoka leo kimuziki na kuwahakikishia mashabiki wake watafurahi.

“Mawe ya Kibongofleva, Kiafrika na Dunia. Nyimbo za mapenzi, maisha, maumivu na starehe. Video za ndani, Afrika na Dunia. Ni mwaka wa tasnia na Taifa kujivunia kuwa na kiumbe kinaichoitwa Nasibu Abdul, Diamond Platunumz, Simba.” alisema Diamond.

Ukichukua kauli hiyo ya Diamond, utaona kuna mgawanyiko wa makundi matatu katika kuachia nyimbo zake, kuna nyimbo zinazolenga soko la Tanzania (Bongofleva), Afrika na Dunia (kimataifa zaidi).

Kwa lugha rahisi, ukimsikia Diamond ametoa nyimbo na Ne-Yo (Marry You), Morgan Heritage (Hallelujah), Omarion (African Beauty) Rick Ross (Waka), hapo analenga zaidi soko la kimataifa, haya ndio anaita mawe ya kidunia.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags