Mfugaji auwawa kwa kutafunwa na mamba

Mfugaji auwawa kwa kutafunwa na mamba

Mfugaji wa mamba huko kaskazini mwa Cambodia amechanwa vipande vipande na Zaidi ya mamba 40 baada ya kuangukia kwenye sehemu walipofungiwa, polisi wamesema.

Luan Nam, mwenye umri wa miaka 72, alikuwa akijaribu kumhamisha mamba mmoja toka kwenye sehemu (cage) yake kisha mamba huyo akaikamata fimbo aliyokuwa nayo Mzee huyo kwa kutumia mdomo wake na kumvutia ndani.

Mamba wengine walimfuata na kumshambulia hadi akapoteza maisha, shirika la habari la AFP limeripoti. Tukio hilo limetokea ijumaa ya wiki iliopita karibu na mji wa Siem Reap.

Mwili wa mzee huyo ulikutwa ukiwa na alama nyingi za meno na mkono wake mmoja ukiwa umenyofolewa. Mhanga huyo alikuwa rais wa chama cha wafugaji wa mamba katika eneo hilo.

Aidha mamba wamekuwa wakifugwa kwaajili ya mayai yao, ngozi na nyama katika nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Asia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags