Mfuasi wa Trump ahukumiwa miaka 4

Mfuasi wa Trump ahukumiwa miaka 4

Mtu mmoja nchini Marekani alifahamika kwa kwajina Richard Barnett, mwenye umri wa miaka 63, alidaiwa kujiunga na kundi la watu waliovamia majengo ya bunge la nchi hiyo mwaka 2021.

Barnett alipigwa picha na mpiga picha wa shirika la habari la AFP, akiwa amekalia kiti kwenye ofisi ya polisi, na picha hiyo ikawa mojawapo ya vielelezo vya uasi.

Akiungana na wafuasi wengine wa Rais Donald Trump, ambao walivamia bunge lilipokuwa likikutana kumuidhinisha Joe Biden, kama Rais ajaye wa Marekani.

Mahakama mjini Washington, ilimtia hatiani Barnett mwezi Januari kwa makosa manane, ikiwa ni pamoja na kuzuia bunge kuidhinisha uchaguzi, kuingia kinyume cha sheria katika majengo ya bunge na kusabaisha fujo na kutumia silaha hatari.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags