Mfahamu zaidi Miss World 2024

Mfahamu zaidi Miss World 2024

Krystyna Pyszková(24) Miss Czech Republic 2022, ndiye mshindi wa taji la Miss World 2024 shindano ambalo lilifanyika Mumbai, India usiku wa kuamkia leo, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Miss Lebanon Yasmina Zaytoun.

Krystyna ambaye ni mwanafunzi wa Chuo kikuu ‘Prague’ na anasomea degrees mbili ya sheria pamoja na utawala wa biashara kwa wakati mmoja huku akiwa anafanya vizuri katika kazi za mitindo

Mlimbwende huyo wa dunia alianzisha taasisi yake aliyoipa jina la ‘Sonta Foundation’ pia alifungua shule ya Kiingereza nchini Tanzania kwa ajili ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu ambapo kuna wakati anajitolea kufundisha, kupitia mradi huo ulimfanikisha kuingia moja kwa moja Top 10 ya Beauty With Purpose.

Aidha ukiachilia mbali kujitolea katika miradi mbalimbali pia aliwahi kuhudhuria katika Chuo cha Sanaa kwa miaka tisa na kumfanya kuvutiwa zaidi na muziki.

Krystyna alipokea taji lake kutoka kwa, Miss World 2022 Karolina Bielawska wa Poland. Hata hivyo anakuwa Miss World wa pili kutoka Jamhuri ya Czech tangu Tatana Kucharova aliposhinda shindano hilo mwaka 2006, anauwezo wa kuongea lugha kwa ufasaha kama Kiingereza, Kipolandi, Kislovakia, na Kijerumani.


Kwa upande wa Tanzania ambayo inawakilishwa na Halima Kopwe imeingia katika Top 10 ya Beauty With Purpose, vilevile Tanzania, Kenya, Uganda zimeingia Top 40 ya jumla, huku Uganda ikifika hadi Top 8 na kushinda taji la Beauty With Purpose Africa






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags