Mfahamu ng’ ombe mfupi kuliko wote duniani

Mfahamu ng’ ombe mfupi kuliko wote duniani

Kama unadhani duniani umeona kila kitu, utakuwa unajiongopea kwani kila siku yanaibuka mambo mpya huku yapo ya zamani pia ambayo bado huyafahamu. Katika ulimwengu ni nadra sana kukutana na wanyama wenye ulemavu japo wapo lakini si wengi.

Kama hujawahi kuona mnyama mwenye udumavu fahamu kuwa amewahi kutokea ng'ombe mfupi zaidi duniani, aitwaye Rani kutoka Bangladesh, ambaye alijipatia umaarufu mkubwa baada ya video na picha zake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, hadi kupelekea aingie kwenye Kitabu cha Rekodi cha Dunia Guinness kama ng'ome mfupi zaidi duniani. 

Ufupi wa ng'ombe huyo unatajwa kuwa na urefu wa 51cm, na uzito wa 26kg. Rani kutokana na umbile lake akiwa na umri wa miaka miwili watu wengi walipendelea kwenda kumtazama na kushangaa maumbile yake. yaliyokuwa yamevunja rekodi ya ng'ombe mfupi zaidi ambayo mwanzo ilishikiliwa na ng'ombe aitwaye Manikyam, kutoka India,ambaye ana urefu wa 61.1 cm.

Hata hivyo mmiliki wa ngombe huyo amewahi kueleza kuwa Rani alikuwa anaogopa ng'ombe wengine hivyo ilimlazimu amuweke tofauti na mifugo mingine.

Ngombe huyo alifariki dunia tarehe 19 Agosti 2021, baada ya kuugua tumbo, kulingana na ripoti za ndani, zilidai kuwa ilisababishwa na kula kupita kiasi na mkusanyiko wa gesi tumboni na hata baada ya kukimbizwa kweye matibabu, madaktari wa mifugo hawakuweza kuokoa maisha yake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags